303 Una Imani ya Kweli Katika Kristo?

1 Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake.

2 Nyinyi huwa na shaka na neno la Kristo na huwezi kulitia katika matendo mara moja. Hii ndio sababu ya nyinyi kutokuwa na imani katika Kristo, na daima kuwa na fikira kumhusu Kristo ndio sababu nyingine ya nyinyi kutoamini Kristo. Kuwa na shaka kila mara kuhusu kazi ya Kristo, kuacha neno Lake kuangukia sikio lisilosikia, kuwa na maoni kwa kila kazi inayofanywa na Kristo na kutoifahamu vizuri kazi hiyo, kuwa na ugumu wa kutupilia mbali fikira zako hata baada ya nyinyi kupewa sababu za kufanya vile, na kadhalika; hizi zote ni dalili za kutoamini zilizochanganyika ndani ya mioyo yenu.

3 Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na kamwe hubaki nyuma, kuna uasi mwingi uliochanganyika ndani ya mioyo yenu. Uasi huu ni doa la uchafu katika imani yenu kwa Mungu. Pengine hamkubaliani na haya, lakini iwapo huwezi kutambua nia yako kutoka kwayo, basi wewe ndiwe utakayeangamia. Kwa maana Mungu hustawisha wale wanaomwamini kwa kweli pekee, wala sio wale walio na shaka na hasa wale wanaomfuata shingo upande licha ya kutowahi kuamini kuwa Yeye ni Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 302 Watu Wanamchukulia Kristo kama Mwanadamu wa Kawaida

Inayofuata: 304 Kuja kwa Mwana wa Adamu Kunawafunua Watu Wote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp