684 Wote Wamtafutao Mungu kwa Kweli Wanaweza Kupata Baraka Zake

1 Watu wanafaa kushirikiana na Mungu vipi katika hatua hii ya kazi Yake? Mungu Anawajaribu watu kwa wakati huu. Haneni neno lolote; Anajificha na Hawasiliani na watu moja kwa moja. Kutoka nje, inaonekana kama Hafanyi kazi, lakini ukweli ni kwamba bado Anafanya kazi ndani ya mwanadamu. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ana maono kwa kufuata kwake maisha, na hana mashaka, hata kama haelewi kazi ya Mungu kikamilifu. Katikati ya majaribu, hata kama hajui ni nini Mungu Anataka kufanya na kazi gani Anataka kukamilisha, unafaa kujua kuwa nia za Mungu kwa wanadamu ni nzuri kila wakati. Ukimfuata na moyo wa kweli, Hatawahi kukuacha, na mwishowe kwa kweli Atakukamilisha, na kuwaleta watu katika mwisho unaofaa.

2 Haijalishi ni vipi Mungu Anawajaribu watu kwa sasa, kuna siku moja ambayo Atawatolea watu matokeo yanayofaa na kuwapa adhabu inayofaa kulingana na kile ambacho wamefanya. Mungu Hatawaongoza watu hadi kituo fulani halafu Awatupe tu kando na kuwapuuza. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwaminifu. Ili watu wapate uzoefu wa kazi ya Mungu, lazima kwanza waelewe kazi Yake ya sasa na kuelewa jinsi wanadamu wanafaa kushirikiana. Hili ni jambo ambalo kila mtu anafaa kuelewa. Lakini lazima uamini kwamba, kwa kuwa kazi ya Mungu imefika hatua fulani, Hatakubali wanadamu wote waangamie hata iweje. Anawapa ahadi na baraka kwa wanadamu, na wale wote wanaomfuata wataweza kupata baraka Yake, na wale wasiomfuata watatupwa nje na Mungu. Hii inategemea kufuata kwako. Lazima uamini kuwa wakati kazi ya Mungu itakapomalizika, kila mtu atakuwa na mwisho unaofaa.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 683 Mtu Hawezi Kuja Kumjua Mungu kwa Kufurahia Neema Yake

Inayofuata: 685 Shikilia Imara Kile Mwanadamu Lazima Afanye

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp