787 Kweli Unamwelewa Mungu?
1 Je, unathubutu kusema kwamba unamjua Mungu? Je, umekuwa na ushughulikaji na Mungu? Je, umejihusisha na Yeye? Je, unajua tabia Yake? Je, unajua ni nini Yeye hupenda? Je, unajua vitu unafanya ambavyo vinaikosea tabia Yake? Je, unajua upotovu ndani yako ambao Yeye huchukia? Je, unajua watu ambao Ameleta tabia Yake yenye haki kwao? Je, unajua ni watu wagani Yeye huchukia? Je, unajua ni masuala yapi unayo ambayo Yeye huchukia zaidi? Kama hujui vitu vyovyote kama hivi, linaonyesha kwamba kwa kweli huna uelewa wa Mungu.
2 Unasema kwamba umemwona Mungu, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha ya Mungu, huelewi tabia Yake, wala huelewi haki Yake. Huna ufahamu wa rehema Zake, na hujui Anachokipenda ama Anachokichukia. Huu si ufahamu wa Mungu. Ikiwa unamjua, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi unafuata tu, mtu fulani anayefuata tu na kufuata umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo