630 Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Kuwasimamia Watu

1 Unapaswa kujua kwamba Mungu kuwakamilisha, kuwatimiza, na kuwapata wanadamu hakuleti kitu chochote ila panga na maangamizi juu ya miili wao, na na vile vile mateso yasiyokoma, moto mkali, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, laana, na majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vinalengwa kwa mwili wa mwanadamu, na mishale yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa mwanadamu. Haya yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si kwa ajili ya binadamu tu, bali pia kwa ajili ya mpango wote, na vile vile kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu.

2 Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho mwanadamu hupitia kinajumuisha mateso na majaribu ya moto, na kuna siku chache sana ambazo ni tamu na zenye furaha au hata hakuna kabisa, ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani sana. Sembuse mwanadamu kuweza kufurahia nyakati za furaha katika mwili, akishinda nyakati nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia ni kuadibu kwa Mungu tu ambako mwanadamu huona kukiwa kusiko kuzuri, na ni kana kwamba hakuna mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Mungu atadhihirisha tabia Yake ya haki, ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kwa njia yoyote inayolazimu, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizo ya Shetani wa zamani!

Umetoholewa kutoka katika “Kusudi la Kuwasimamia Binadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 629 Umeacha Fikira Zako za Kidini?

Inayofuata: 631 Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp