Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

959 Kubadili Tabia Yako Kunaanza na Kuelewa Asili Yako

1 Unaanzia wapi katika kugeuza tabia yako? Je, mwajua? Huanza na kufahamu asili yako mwenyewe. Hili ndilo muhimu. Mnaelewa vipi asili ya mwanadamu? Kuifahamu asili yako kunamaanisha kuchambua kina cha nafsi yako kwa kweli; kunahusu kile kilicho katika maisha yako. Ni mantiki ya Shetani na mitazamo mingi ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo daima; yaani, ni maisha ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo. Ni kwa kufichua tu sehemu za kina kabisa za nafsi yako ndio unaweza kuifahamu asili yako. kwa mfano, mitazamo ya watu kuhusu vitu, mbinu na malengo ya watu katika maisha, maadili ya maisha na mitazamo kuhusu maisha ya watu, pamoja na mitazamo kuhusu vitu vyote vinavyohusiana na ukweli. Hivi ni vitu vyote vilivyo ndani kabisa ya nafsi za watu na vina uhusiano wa moja kwa moja na mgeuzo wa tabia.

2. Binadamu wapotovu wana mtazamo upi kuhusu maisha? Ni huu: “Kila mtu ajali maslahi yake, akiwaacha wasio na bahati kwa majaliwa yao.” Watu wote wanaishi kwa ajili yao wenyewe, na kusema kwa ufupi, wanajali tu kuhusu kulisha na kuvisha miili yao. Maisha yao hayana kiwango chochote cha umuhimu ama thamani. Mitazamo ya maisha ni ile unayotegemea ili kusalia na kuishi; ni ile ambayo ni sababu yako ya kuishi, na jinsi unaishi, Hivi vyote ni dutu ya nafsi ya binadamu. Kwa kuchambua asili za watu, utaona kwamba watu wote wanampinga Mungu. Wote ni mashetani na hakuna mtu mzuri kwa kweli. Ni kwa kuchambua asili za watu tu ndio unaweza kujua kweli dutu na upotovu wa mwanadamu na kufahamu watu wanamilikiwa na nini hasa, kile watu wanakosa kweli, kile wanapaswa kujizatiti nacho, na jinsi wanapaswa kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kuweza kuchambua kweli asili za watu si rahisi. Hakutafaulu bila ukweli na uzoefu.

Umetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:Mabadiliko Katika Tabia Hasa ni Mabadiliko Katika Asili

Inayofuata:Kuijua Asili Yako Mwenyewe ni Muhimu kwa Badiliko Katika Tabia

Maudhui Yanayohusiana