898 Mungu Anafarijiwa Watu Wanapoyaacha Makosa Yao
1 Katika siku za nyuma, watu wengine wamefukuzwa kwa kufanya mambo kadhaa mabaya na kanisa limewakataa. Wanatangatanga kwa miaka kadhaa, na kisha wanarudi. Ni vizuri kwamba hawajatoroka kabisa; kwa kuwa hawajatoroka kabisa, wana fursa na tumaini la kuokolewa. Hii ni nadra na ya thamani. Bila kujali jinsi Mungu huwafinyanga watu na bila kujali jinsi Mungu huwatendea watu, huwachukia watu, au huwakirihi watu, kama utakuja wakati ambapo watu wanaweza kugeuka, basi Mimi nitapata faraja maalum; hii ina maana kwamba watu bado wana wingi wa Mungu ndani ya mioyo yao, hajapoteza mantiki ya kibinadamu kabisa, hawajapoteza ubinadamu kabisa, bado wana nia ya kumwamini Mungu, na wanatarajia kumkubali na kurudi kwa Mungu. Bila kujali ni nani anayekimbia, wakirudi, na familia hii bado iko katika mioyo yao, Mimi nitakuwa mwepesi wa upendo kidogo na kuhisi faraja; hata hivyo, wale ambao hawarudi kamwe ni wa kudharaulika. Ikiwa wanaweza kurudi na kuanza kuamini katika Mungu kwa kweli, moyo Wangu utajazwa hasa na furaha.
2 Katika Enzi ya Neema, Yesu alikuwa na huruma na neema kwa watu. Kama kondoo mmoja angepotea miongoni mwa mia moja, angewaacha tisini na tisa na kumtafuta yule mmoja. Fungu hili halielezi tendo la kimitambo, siyo kanuni, lakini linaonyesha nia ya Mungu kwa wanadamu, lengo la dharura la Mungu la kumwokoa binadamu, na mapenzi ya kina ya Mungu kwa wanadamu. Si njia ya kutenda, lakini ni tabia Yake na akili Yake. Kwa hiyo, watu wengine huondoka kwa mwaka mmoja au nusu mwaka, au wana udhaifu mwingi na kuelewa kwingi visivyo. Baadaye, ikiwa wataamka kwa ukweli na wanaweza kuwa na ufahamu na kugeuka na kurudi kwenye njia sahihi, hasa Mimi nitafarijiwa na kupendezwa na hili. Kuwa na uwezo wa kusimama katika dunia ya sasa na enzi ya raha za kimwili na uovu, kuwa na uwezo wa kumkubali Mungu, na kuwa na uwezo wa kurudi kwa njia sahihi na kurudi ni mambo ambayo kwa kweli huleta faraja na ni ya kusisimua.
Umetoholewa kutoka katika “Watu Ambao Hufanya Madai Daima kwa Mungu Ndio Wenye Busara Kidogo Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo