437 Geuza Moyo Wako kwa Mungu Kikamilifu ili Kuweza Kumpenda

1 Watu wanapowasiliana na Mungu na mioyo yao, mioyo yao inapoweza kumgeukia Yeye kikamilifu, hii ni hatua ya kwanza ya upendo wa wanadamu kwa Mungu. Ikiwa unataka kumpenda Mungu, lazima kwanza uweze kugeuza moyo wako Kwake. Kugeuza moyo wako kwa Mungu ni nini? Ni wakati ambapo kila kitu unachofuatilia ndani ya moyo wako ni kwa ajili ya kumpenda na kumpata Mungu. Bali na Mungu na maneno Yake, hakuna takriban kitu chochote kingine ndani ya moyo wako. Hata kama vipo, haviwezi kuumiliki moyo wako, na hufikirii juu ya matazamio yako ya baadaye lakini unafuatilia tu kumpenda Mungu. Wakati huo utakuwa umegeuza moyo wako kwa Mungu kabisa.

2 Ukimwomba Mungu na kula na kunywa maneno Yake kila siku, unafikiria kila mara kuhusu kazi ya kanisa, ukifikiria juu ya mapenzi ya Mungu, ukitumia moyo wako kumpenda Yeye kwa uhalisi na kuridhisha moyo Wake, basi moyo wako utakuwa wa Mungu. Njia ya mtu kutimiza upendo wa kweli kwa Mungu na kujua tabia ya Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu. Baada ya kutoa moyo wao wa kweli kwa Mungu, wataanza kuingia katika uzoefu wa maisha, na hivyo tabia yao itaanza kubadilika, upendo wao kwa Mungu utakua polepole, na ufahamu wao wa Mungu utaongezeka pia polepole.

3 Kugeuza moyo wa mtu kwa Mungu ni sharti la mwanzo la yeye kuingia katika njia sahihi, la kumfahamu Mungu, na la kutimiza upendo wa Mungu. Siyo alama ya kukamilisha wajibu wake ya kumpenda Mungu, wala siyo alama ya kuwa na upendo halisi Kwake. Njia ya pekee ya mtu kutimiza upendo halisi kwa Mungu ni kuurudisha moyo wake kwa Mungu, ambacho pia ni kitu cha kwanza mmoja wa uumbaji Wake anapaswa kufanya. Wale wanaompenda Mungu wote ni watu wanaotafuta uzima, yaani, watu wanaofuatilia ukweli na watu wanaomtaka Mungu kweli; wote wana nuru ya Roho Mtakatifu na wamesisimuliwa n na Yeye. Wote wanaweza kuongozwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 436 Moyo Wako Umemrudia Mungu?

Inayofuata: 438 Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp