434 Elekeza Moyo Wako Kwa Mungu Ili Uhisi Kupendeza Kwake

1 Ikiwa unaweza kutia ukweli katika vitendo kiasi cha kumridhisha Mungu, basi moyo wako utamgeukia Mungu. Kadiri utakavyozidi kumwomba Mungu na kuwasiliana kwa karibu na Mungu, ndivyo utakavyozidi kugundua kile kinachopendeka kumhusu. Ikiwa, ndani kabisa, uko radhi kwa kweli kumridhisha Mungu, basi Atakutwika mzigo Wake, na kisha utapata upambanuzi hata zaidi wa kupendeza Kwake kukuu. Hii itakuwezesha kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, na utahisi ndani yako kabisa kwamba Yeye ni wa kupendeka. Mara utakapoweza kumpenda Mungu kwa dhati, utahisi kupendeza Kwake zaidi na zaidi—na vile vile kustahili Kwake upendo wa binadamu—na kisha utaweza kumtii na kumwabudu kwa hiari.

2 Wakati huo, utaweza kupendezwa na Mungu ndani kabisa ya moyo wako; utataka kuimba sifa Zake na kutoa sifa nyingi mno za shukrani juu Yake. Unapokuwa ukimsifu sana kutoka ndani kabisa ya nafsi yako, hakuna mtu atakayeweza kukuzuia. Utakapohisi jinsi Mungu anavyopendeka kabisa, shukrani zako na upendezwaji wako Kwake vitakua zaidi na zaidi, na kisha utakuwa na dhana na mawazo yasiyofaa machache zaidi na zaidi kumhusu; kisha Shetani ataacha kuwa na fursa za kufanya kazi ndani yako. Utakapofika hapa, utakuwa umeondokana kabisa na ushawishi wa Shetani wa kifo, na moyo wako utakombolewa kabisa na kuwa huru.

Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu

Iliyotangulia: 433 Unapoutoa moyo wako kwa Mungu

Inayofuata: 435 Toa Moyo Wako Mbele za Mungu Ikiwa Wamwamini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp