197 Kupata Mwili Kuwili kwa Mungu ni kwa Ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

1 Miili hiyo miwili ya Mungu ya nyama imekuwepo ili kumshinda Shetani, na pia imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa njia bora zaidi. Hilo ni kwa sababu yule anayefanya vita na Shetani anaweza tu kuwa Mungu, awe ni Roho wa Mungu au ni mwili wenye nyama wa Mungu. Kwa kifupi, yule anayefanya vita na Shetani hawezi kuwa ni malaika, sembuse kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana uwezo wa kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanyia kazi maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja duniani binafsi kumwokoa mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi apate mwili—yaani, lazima Yeye binafsi achukue mwili, na kwa utambulisho Wake wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeshindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingekwisha.

2 Vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa tu na Mungu Mwenyewe, na itakuwa tu vigumu kwa mwanadamu kupigana vita hivyo. Wajibu wa mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi kama vile kuumba mbingu na dunia, wala, zaidi ya hayo, hawezi kutekeleza kazi ya kupigana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote. Pambazuko la kila enzi mpya ni mwanzo mpya katika vita na Shetani, ambapo kupitia hiyo mwanadamu anaingia akiwa mpya zaidi, ulimwengu wa kupendeza zaidi na enzi mpya ambayo inaongozwa na Mungu Mwenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 196 Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Kazi ya Mungu Katika Mwili

Inayofuata: 198 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu Mara Mbili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp