559 Elewa Hali Zako za Kweli ili Ujielewe

1 Kama watu wanafaa kujielewa, ni lazima waelewe hali zao za kweli. Kipengele cha muhimu zaidi katika kuielewa hali ya mtu ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zake na mawazo yake. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa. Ikiwa unaweza kudhibiti fikira zako, unaweza kudhibiti vitu vilivyo nyuma yazo. Watu hawawezi kuzidhibiti fikira na mawazo yao, lakini wanapaswa kujua fikira na mawazo haya hutoka wapi, nia zao ni gani, jinsi fikira hizi na mawazo haya huzalishwa, ni nini kinachozidhibiti na ni nini asili yazo.

2 Baada ya tabia yako kubadilika, fikira na mawazo yako, tamaa ambazo moyo wako unatafuta, na maoni yako juu ya vitu unavyokimbiza—ambavyo vimefanyizwa kutoka kwa sehemu zako ambazo zimebadilishwa—zitakuwa tofauti. Hizo fikira na mawazo zinazotoka kwa sehemu zako ambazo hazijabadilika, vitu ambavyo wewe huvielewi kwa dhahiri, na vitu ambavyo hujabadilisha na uzoefu wa ukweli ni vichafu, vyenye taka na visivyovutia. Watu siku hizi ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa miaka kadhaa wana hisia na ufahamu kiasi wa mambo haya. Watu ambao wamepitia kazi ya Mungu kwa kipindi cha muda mfupi bado hawaelewi mambo haya; Bado hawajui udhaifu wao uliko na ni sehemu gani ambazo ni rahisi kwao kuanguka!

3 Hamjui kwa sasa nyinyi ni mtu wa aina gani, na watu wengine wanaweza kuona kwa kiasi fulani nyinyi ni aina gani ya watu, ambapo hamuwezi kuhisi. Hamuwezi kwa dhahiri kutofautisha fikira zenu za kawaida au nia, na hamuelewi kwa dhahiri ni nini asili ya mambo haya. Jinsi unavyokielewa kipengele kwa kina, ndivyo utakavyozidi kubadilika katika kipengele hicho; hivyo, mambo unayoyafanya yatakuwa kwa mujibu wa ukweli, utakuwa na uwezo wa kuyatimiza mahitaji ya Mungu, na utakuwa karibu na mapenzi ya Mungu. Ni kwa kutafuta kwa njia hii tu ndipo utaweza kupata matokeo.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 558 Jielewe Kulingana na Maneno ya Mungu

Inayofuata: 560 Jinsi ya Kuelewa Asili ya Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

1Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu,kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa...

85 Njia Yote Pamoja na Wewe

1Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani.Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga.Maneno...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki