558 Jielewe Kulingana na Maneno ya Mungu

1 Watu wana ufahamu wa juujuu sana kuhusu asili yao wenyewe, na kuna tofauti kubwa kati ya hili na maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo. Watu hawana ufahamu wa kimsingi au wa halisi wa wao wenyewe; badala yake, wao wanalenga na kutenga nguvu zao kwa matendo na maonyesho ya nje. Hata kama mtu fulani angelisema jambo mara chache kuhusu kujifahamu, halingekuwa la kina sana. Hakuna mtu aliyewahi kufikiria kwamba yeye ni aina hii ya mtu au ana asili ya aina hii kutokana na kulitenda jambo kama hili au kulifunua jambo. Mungu ameifunua asili na kiini cha mwanadamu, lakini wanadamu wanafahamu kwamba njia yao ya kuyatenda mambo na njia yao ya kusema ni yenye mawaa na yenye kasoro; kwa hiyo, ni kazi yenye kutumia juhudi nyingi kwa watu kutia ukweli katika vitendo.

2 Watu wanafikiria kwamba makosa yao ni udhihirisho wa muda tu ambao unafunuliwa bila kujali, badala ya kuwa ufunuo wa asili yao. Watu ambao hujiona kwa namna hii hawauweki ukweli katika vitendo, kwa sababu hawawezi kukubali ukweli kama ukweli na hawatamani ukweli; kwa hiyo, wakati wanatia ukweli wao katika vitendo wanaifuata tu sheria kwa uzembe. Watu hawaoni asili yao wenyewe kama iliyo potovu sana, na wanaamini kwamba wao si wabaya sana kiasi kwamba wanapaswa kuangamizwa au kuadhibiwa. Wao hufikiri kuwa si jambo kubwa kudanganya mara kwa mara, na hujiona kuwa bora zaidi kuliko jinsi walivyokuwa zamani; hata hivyo, kwa kweli wako mbali sana na kiwango kinachohitajika, kwa sababu watu wana matendo fulani tu ambayo kwa nje hayakiuki ukweli, wakati kwa kweli hawatii ukweli katika vitendo.

Umetoholewa kutoka katika “Kuifahamu Asili ya Mtu na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 557 Unaijua Asili Yako?

Inayofuata: 559 Elewa Hali Zako za Kweli ili Ujielewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp