796 Matokeo ya Kuielewa Tabia ya Mungu

1 Kupata kujua dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole na bila kujua, utaanza kujua dutu ya Mungu. Wakati umeingia katika maarifa haya, utajipata ukisonga mbele hadi kwa hali iliyo ya juu na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unahisi hakuna mahali pa kujificha. Wakati huo, kutakuwa na machache zaidi na zaidi katika mwenendo wako ya kukosea tabia ya Mungu, moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utakua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya wanadamu kuingia katika hali nzuri.

2 Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Mnaposhughulika huku na kule kwa ajili ya majaaliwa yenu, ni nani angefikiria kujaribu kujua dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtazikosea amri za utawala bila kujua, kwani mnafahamu kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi wa makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muelewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa?

3 Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi nitakayowaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku ifike ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 795 Uhuru Hupatwa kwa Kujua Amri ya Mungu

Inayofuata: 797 Kazi ya Mungu Haiwezi Kueleweka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp