990 Wale Watu Wasiotubu Walionaswa Katika Dhambi Hawawezi Kuokolewa

1 Sasa, iwapo ufuatiliaji wenu umekuwa wa kufaa au la linatathminiwa na kile mlicho nacho sasa. Hiki ndicho kinachotumiwa kuamua matokeo yenu; yaani, matokeo yenu yanafichuliwa katika kujitolea mlikofanya na mambo ambayo mmefanya. Matokeo yenu yatadhihirishwa na ufuatiliaji wenu, imani yenu na mambo ambayo mmefanya. Kati yenu nyote, kuna wengi ambao tayari hawawezi kuokolewa, kwani leo ndiyo siku ya kufichua matokeo ya watu, na Sitakanganyikiwa katika kazi Yangu; Sitawaongoza wale wasioweza kuokolewa kabisa katika enzi ifuatayo. Kutakuwa na wakati ambapo kazi Yangu itakuwa imekamilika. Sitafinyanga maiti hizo ambazo haziwezi kuokolewa hata kidogo; sasa ndizo siku za mwisho za wokovu wa mwanadamu, na Sitafanya kazi isiyo ya maana.

2 Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno ya safihi; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa mengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa?

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 989 Unauelewa Mtazamo wa Mungu Anapomwadhibu Mwanadamu

Inayofuata: 991 Unapaswa Kuyachukuliaje Maneno na Vitendo Vyako Mwenyewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp