305 Hustahili Kuwasiliana na Mungu kwa Mantiki kama Hiyo

1 Ingekuwa bora kwenu kuweka juhudi zaidi kwa ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata fadhili kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu ni chukizo sana Kwake? Kwa nini maneno yenu yanachochea chuki Yake? Punde ambapo mmeonyesha uaminifu kidogo, nyinyi mnajisifu wenyewe, na mnadai malipo kwa ajili ya mchango mdogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kumdharau Mungu baada ya kufanya kazi ndogo. Mnataka utajiri, zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kutendewa kwa heshima. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Kuna chochote kinachostahili sifa katika maneno na matendo yenu?

2 Mkijua vyema kwamba mnamwamini Mungu, hata hivyo ninyi hamwezi kulingana na Mungu. Kweli mnajua vyema kwamba hamstahili hata kidogo. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imepunguka kiasi kwamba hamwezi tena kujizuia? Na hisia kama hii, mnastahili vipi kushirikiana na Mungu? Je, kufikia hapa nyinyi hamjionei hofu? Tabia yenu tayari imepunguka kiasi kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Hali ikiwa hivi, je, imani yenu si ya kuchekesha? Imani yenu si ya kipuuzi? Ni jinsi gani utashughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kutembelea?

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 304 Kuja kwa Mwana wa Adamu Kunawafunua Watu Wote

Inayofuata: 306 Binadamu Wapotovu Hawastahili Kumwona Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp