752 Thamani ya Maisha ya Ayubu

1 Je, Ayubu aliishi maisha ya thamani? Thamani yake ilikuwa wapi? Kutoka katika mtazamo wa binadamu, aliwawakilisha wanadamu ambao Mungu alitaka kuokoa, kwa kuwa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu. Alitimiza wajibu ambao ulistahili kutimizwa na kiumbe wa Mungu, na kuweka mfano halisi wa kuigwa, na kutenda kama kielelezo, kwa wale wote ambao Mungu angependa kuwaokoa, akiruhusu watu kuona kwamba inawezekana kabisa kushinda Shetani kwa kumtegemea Mungu. Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa ndani ya uwezo wake wa kumcha Mungu, kumwabudu Mungu, kutolea ushuhuda vitendo vya Mungu, na kusifu vitendo vya Mungu, kumpa Mungu tulizo na kitu cha kufurahia.

2 Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa pia kwa namna ambavyo, kabla ya kifo chake, Ayubu alipitia majaribio na kushinda Shetani, na akawa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu, akimtukuza Mungu miongoni mwa wanadamu, akiutuliza moyo wa Mungu na kuruhusu moyo wa Mungu wenye hamu kuyaona matokeo, na kuliona tumaini. Ushuhuda wake uliweka mfano wa kufuatwa kutokana na uwezo wake wa kusimama imara katika ushuhuda wa Mungu, na kuweza kumwaibisha Shetani kwa niaba ya Mungu, katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu.

3 Ayubu alileta tulizo kwa moyo wa Mungu, alimpa Mungu kionjo cha furaha ya kutukuzwa, na akaanzisha mwanzo mzuri kwa mpango wa usimamizi wa Mungu. Na kuanzia hapo kuenda mbele jina la Ayubu likawa ishara ya utukuzaji wa Mungu na ishara ya kushinda kwa wanadamu dhidi ya Shetani. Kile Ayubu aliishi kwa kudhihirisha wakati wa maisha yake na ushindi wake wa kipekee dhidi ya Shetani milele utabakia ukifurahiwa mno na Mungu na utimilifu wake, unyofu, na hali yake ya kumcha Mungu itaheshimiwa na kuigwa na vizazi vitakavyokuja. Milele atafurahiwa mno na Mungu kama johari lisilo na makosa, wala dosari, na pia ndivyo alivyo na thamani ya kuthaminiwa sana na binadamu!

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 751 Ayubu Alitumia Maisha Yake Yote Kutafuta Kumjua Mungu

Inayofuata: 753 Yote Anayofanya Mungu ni Kumwokoa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp