Swahili Christian Testimony Video "Moyo Uliopotea Waja Nyumbani" Wokovu wa Ajabu wa Mungu

06/02/2018

Tangu alipokuwa mdogo, Novo alimwamini Bwana Yesu, kama mama yake tu. Hata kama alisoma Biblia, kuomba, na kuhudhuria mahubiri mara kwa mara, mara nyingi hangeweza kujizuia bali kufuata mielekeo mibaya ya dunia, kutamani raha za mwili, na kudanganya na kusema uwongo…. Alikusudia mara nyingi kuyaacha maisha ya aina hiyo ya kuzunguka katika kutenda dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi. Hata hivyo, kila wakati hakufaulu. Baadaye Novo alipokuwa akifanya kazi nchini Taiwan alisikia injili ya ufalme, na kwa kuyasoma maneno Yake Mwenyezi Mungu alifikia hitimisho kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu, na kuwa kazi Yake ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho ina uwezo wa kusuluhisha kikamilifu tatizo la asili ya mwanadamu ya dhambi. Hivyo, alikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kwa moyo uliojaa furaha. Miaka miwili baada ya hayo, Novo alirudi nchini Ufilipino na kuanza kutekeleza wajibu wake katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Alipata lengo na mwelekeo wake katika maisha, na kutoka wakati huo na kuendelea moyo wake uliopotea mwishowe ukaja nyumbani.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp