Swahili Gospel Video | "Nuru ya Mapambazuko"

21/06/2018

Kama mtoto, Yangwang aliwafuata wazazi wake katika imani yao kwa Bwana, na kama mtu mzima alihudumia Bwana kanisani. Mnamo 2013, kanisa lake lilijiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni ambalo hutetea uunganishwaji wa kanisa kote ulimwenguni na wingi wa dini. Akisadiki kwamba kusisitiza kwa wachungaji na baraza la wazee wake katika kujiunga na Baraza kulikuwa kuondoka kwa njia ya Bwana na hakuwiani na moyo wa Bwana, hatimaye aliliacha dhehebu lake na kuanza kulitafuta kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini, baada ya kuyatembelea makanisa mbalimbali, aligundua kwamba madhehebu yote yalikuwa na ukiwa, na kwamba hakukuwa na nuru katika mahubiri ya wachungaji na mabaraza yao ya wazee. Hakuweza kupata utoaji wa uzima, na roho yake ilikuwa ikinyauka na kugeuka kuwa giza. Kwa maumivu yake, mara nyingi angemuita Bwana, akimwomba Bwana arudiharaka. … Siku moja, alienda mtandaoni kutafutataarifa kuhusu kurudi kwa Bwana, pale alipoiona video ambayo maneno ya Mwenyezi Mungu yalisomwa. Maneno ya Mwenyezi Mungu yaliishtua nafsi yake. Alihisi yalikuwa na mamlaka na nguvu na yalionekana kama sauti ya Mungu. Ili kuamua kama Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, alianza kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikia ushirika wa watoaji ushuhuda, aliutatua mkanganyo wake. Aligundua kwamba neno lote la Mwenyezi Mungu ni la ukweli, kwamba kwa hakika ni sauti ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu ambaye kurudi kwake alikuwa akisubiri kwa miaka mingi akiutamani. Kwa kuwa, amelisoma neno la Mungu kila siku, hivyo basi kuilisha nafsi yake yenye kiu, na kupokea kwa kweli maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi.

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp