Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

"Imani katika Mungu" (3) - Je, Kazi ya Mungu na Kuonekana kwa Mungu Kunaleta Nini katika Jamii ya Dini?

Dondoo za Filamu   239  

Utambulisho

Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili na kuonekana ili kufanya kazi Yake, nguvu za uovu za Shetani hupinga na kulaani njia ya kweli kwa ghadhabu. Kwa njia hii, vita vinatokea ndani ya dunia ya kiroho ambavyo hugawanya na kufunua ulimwengu wa dini. Bwana Yesu alisema, “Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani: sikuja kuleta amani, bali upanga”(Mathayo 10:34). Wakati ambapo Bwana Yesu alionekana na kufanya kazi katika Enzi ya Neema, dini ya Kiyahudi iligawanyika katika vikundi vingi. Sasa kwa kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ulimwengu wa dini unapatwa na mfichuo mkubwa; ngano na magugu mwitu, kondoo na mbuzi, wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu, na watumishi wazuri na watumishi wabaya —wote wanafunuliwa, kila mmoja na aina yake. Hekima ya Mungu na maajabu kweli ni ya kina sana!