Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu

23/04/2018

Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika. Huko, mjadala ulijitokeza miongoni mwa Zheng Xun na wafanyakazi wenzake kuhusu kama muumini katika Mungu anapaswa kutii wale walio madarakani au la. Yu Congguang alitoa ushirika kwa kuzingatia suala hili na kuondoa kuchanganyikiwa kwao. Ushirika wa Yu Congguang ulikuwa wa manufaa sana kwao, na wote wakaanza kutafuta na kujifunza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hata hivyo, Mzee Sun kutoka kanisa la mahali pale alipopata habari kwamba Yu Congguang alikuwa shahidi kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, alifanya kila kitu ambacho angeweza kulizuia kanisa na kuwazuia wafuasi kutafuta njia ya kweli. Sun alikwenda katika nyumba moja hadi nyingine kumtafuta Yu Congguang, na hata kuwahamasisha wafuasi kumripoti Yu kwa polisi na kumkamata ...

Huku akifuatwa na kuteswa na serikali ya CCP na Mzee Sun, Yu Congguang alimwomba Mungu kwa dhati. Alimtegemea Mungu na akakusudia mwenyewe kuwaongoza mbele ya Mungu waumini wa kweli kutoka kanisa la mahali pale ambao walitafuta na kuchunguza njia kweli. Baada ya kupitia vizuizi kadhaa, Yu Congguang, Zheng Xun na wengine walilazimika kuwa wamakinifu, wakijificha katika matete, sehemu za chini za nyumba, na mapango ili kufanya ushirika kuhusu neno la Mwenyezi Mungu. ... Kwa sababu Zheng Xun na wengine kadhaa walikuwa wamepeleleza Umeme wa Mashariki, Mzee Sun aliwachukulia wao kama maadui, na ghafla kanisa likagawanyika katika makundi mawili. Kwa sababu hii, Zheng Xun na washiriki wenzake wa kanisa walihuzunika na kuchanganyikiwa. Yu Congguang alifanya ushirika nao kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu ili kutatua rabsha yao. Yeye pia alifanya ushirika kuhusu maana ya kuwa na imani katika Mungu, na jinsi ya kuwa na imani ambayo Mungu atasifu na kutukuza. Hatimaye, Zheng Xun na wengine walianza kuelewa ukweli, na kuchanganyikiwa kwao, matatizo yao, na michepuko ilitatuliwa. Mioyo yao ilikombolewa, na walitanafusi kwa kina, kwani baada ya miaka mingi ya kuamini katika Bwana, hatimaye waligundua maana ya kweli ya "imani katika Mungu." ...

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp