Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 161

23/07/2020

Sasa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya mwanzoni, wala halazimishi watu kwenda mbele. Wakati wa hatua hii ya kazi, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Wameona upendo wa Mungu, na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amevunjika roho, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo kidogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka kwa wema na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati wanadamu hawamtii Mungu ama wanampinga Yeye, ama wanapofichua upotovu wao, Mungu hataonyesha huruma kuwarudi na kuwafundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua, na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia yao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote la gharama hii ama mambo haya Mungu anafanya, ilhali yote ambayo anafanya kwa kweli inafanywa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimili wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu yanaruhusu watu kuja kujua polepole upotovu wa wanadamu na kiini chao cha kishetani. Kile ambacho Mungu anapeana, kutia nuru Kwake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, kile wanachoishia, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Je, mnajua? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya uasherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kufuatilia ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na katika maneno Yake kwa njia njema kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata uchaji wa Mungu na uepukaji wa uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp