Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Ufalme” | New Jerusalem Has Come Down Out of Heaven

15/08/2018

Ufalme, mji wa watakatifu, ufalme wa Kristo.

Katika ufalme, utajiri na utukufu wa Mungu hudhihirishwa.

Umeme unatoka Mashariki na kuangaza hadi Magharibi.

Mwanga wa kweli uko hapa, neno la Mungu limeonekana katika mwili.

Mwokozi amesharudi, akishuka juu ya wingu jeupe.

Watakatifu leo ​​wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi ili kumwabudu Mungu.

Watakatifu wa zamani wamefufuka tena kusimama imara katika siku za mwisho.

Watakatifu wanateswa kwa ukatili nchini China, nchi ya mapepo.

Kwa miaka elfu sita ya historia, watakatifu wamemwaga damu na kulia machozi,

wasiweze kurudi nyumbani, wakiyumba kutoka sehemu moja hadi nyingine,

bila mahali pa kulaza kichwa chao.

Katika shimo la taabu, giza ambalo hakuna jua linaloangaza, makundi ya Shetani yanacheza.

Miaka sita elfu ya vita, damu na machozi inakaribisha kuja kwa ufalme.

Tunasikia sauti ya Mungu na tunanyakuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi.

Tunapitia hukumu ya Kristo na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwana Kondoo.

Tunafikia utakaso kwa maneno ya Mungu na kuona haki na utakatifu Wake.

Kushindwa na kukamilishwa na maneno ya Mungu, tunapata wokovu Wake wa si ku za mwisho.

Ninasifu na kuimba kwa sauti kubwa juu ya matendo ya ajabu ya Mwenyezi Mungu.

Ninatoa sifa zisizoisha juu ya tabia ya haki ya Mwenyezi Mungu.

Ninafurahi na kuruka kwa ajili ya hekima na kudura ya Mwenyezi Mungu.

Siwezi kupenda unyenyekevu na kjificha kwa Mwenyezi Mungu vya kutosha.

Kushindwa kulipa upendo wa Mungu, moyo wangu huhisi machungu na hatia.

Mimi ni mtu mwenye moyo na roho, hivyo kwa nini nisiweze kumpenda Mungu?

Mungu ni msaada wangu, kuna nini cha kuhofu? Ninaahidi maisha yangu kupigana na Shetani mpaka mwisho.

Mungu anatuinua, tunapaswa kuacha kila kitu nyuma na kupigana kuwa na ushuhuda kwa Kristo.

Mungu atatekeleza mapenzi Yake duniani.

Nitaandaa upendo wangu na uaminifu na kuvitoa kwa Mungu.

Nitakaribisha kurudi kwa Mungu kwa shangwe atakaposhuka katika utukufu,

na kukutana na Yeye tena ufalme wa Kristo utakapofanyika.

Kristo amekuja duniani kama mwanadamu, amevaa mwili kupigana vita.

Anafuta machozi ya watakatifu, na kuwaokoa kutoka kwa Shetani.

Tunawachukia mapepo, maadui wachungu wa Mungu.

Uhalifu wao wa umwagaji damu hauwezi kuhesabiwa, ukiacha kumbukumbu za wazi sana.

Tunajazwa na chuki kali, na hasira yetu haiwezi tena kuzuiwa.

Tunamkana Shetani, tunamwombea Shetani ahukumiwe na mapepo waadhibiwe vikali.

Hatuwezi kuwa na upatanisho, tunaahidi kupigana nao hadi mwisho.

Uharibifu tu wa ufalme wa Shetani ndio unaweza kupoza chuki iliyo mioyoni mwetu.

Kutokana na shida kunatokea askari wengi wenye ushindi mzuri.

Sisi ni washindi na Mungu na tunakuwa ushahidi wa Mungu.

Itazame siku ambayo Mungu anapata utukufu, inakuja na nguvu isiyoweza kushindwa.

Watu wote wanatiririka kwenye mlima huu, wakitembea katika nuru ya Mungu.

Utukufu wa ufalme usio na kifani lazima uwe wazi duniani kote.

Siku za usoni za ufalme zinang’aa na zisizo na kikomo; Mungu anakuja Mwenyewe ulimwenguni kuchukua mamlaka.

Watakatifu wa zamani wanafufuka tena kutoka mautini na kufurahia baraka za milele.

Siku za usoni za ufalme zinang’aa na zisizo na kikomo; Mungu anakuja Mwenyewe ulimwenguni kuchukua mamlaka.

Watakatifu wa zamani wanafufuka tena kutoka mautini na kufurahia baraka za milele.

Ufalme, mji wa watakatifu, ufalme wa Kristo.

Katika ufalme, utajiri na utukufu wa Mungu hudhihirishwa.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi