896 Mungu Daima Anamsubiri Mwanadamu Kumrudia

1 Ni mara nyingi Nimemwita mwanadamu kwa Roho Wangu, lakini matendo yake huwa ni kama amechomwa kisu na Mimi, anahusiana nami kwa umbali, katika hofu kubwa kuwa Nitamwongoza kwenda ulimwengu mwingine. Kwa mara nyingi Nimepeleleza ndani ya moyo wa mwanadamu, lakini anabaki bila ufahamu kabisa, akiwa na hofu kubwa kabisa kuwa Nitaingia nyumbani mwake na kuchukua fursa hiyo kumnyang’anya mali yake yote. Kwa hivyo, ananifungia nje, kuniacha bila chochote ila mlango uliofungwa na kukazwa na kuniacha nje kwenye baridi. Ni mara nyingi mwanadamu ameanguka na Nimemwokoa, lakini baada ya kuamka ananiacha mara moja, bila kuguswa na upendo Wangu, mwanadamu kunipiga macho ya hadhari; Sijawahi pasha joto moyo wa mwanadamu.

2 Mwanadamu ni kiumbe kikatili kisichokuwa na hisia. Hata kama amepashwa joto na kumbatio Langu, kamwe hajawahi guswa na jambo hili. Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani. Hajawahi thamini upendo Wangu wa binadamu. Hana nia ya kunikaribia, akipendelea kukaa katika milima, ambapo anavumilia tishio la wanyama pori—lakini bado hana nia ya kuchukua makao ndani Yangu. Simshawishi mwanadamu yeyote: Ninafanya tu kazi Yangu. Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 20” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 895 Mapenzi ya Mungu kwa Wanadamu Hayatabadilika Kamwe

Inayofuata: 897 Mungu Anataka Kumwokoa Mwanadamu kwa Kiasi Kikubwa Mno Iwezekanavyo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp