603 Unaitembea Njia ya Paulo Wakati Hufuatilii Ukweli

1 Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: “Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri.” Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo.

2 Kumwamini Mungu kwa mtu wa aina hii ni kitendo cha kazi ya siku zote, na katika akili yake anahisi kuwa kadri anavyofanya, ndivyo itakavyothibitisha zaidi kuwa ni mwaminifu kwa Mungu, kwamba kadri anavyofanya ndivyo Mungu ataridhika zaidi, na kwamba kadri anavyofanya ndivyo anavyopaswa zaidi kupata taji mbele za Mungu, na hakika atapata baraka kubwa zaidi katika nyumba ya Mungu. Anahisi kwamba kama anaweza kuvumilia mateso, kuhubiri, na kufa kwa ajili ya Kristo, kama anaweza kuyadharau maisha yake mwenyewe, na kama anaweza kukamilisha wajibu wote ambao Mungu alimwaminia nao, basi atakuwa mtu mwenye kubarikiwa zaidi na Mungu, yule anayepata baraka nyingi zaidi, na hakika atapokea taji.

3 Na ilikuwa chini ya uongozi wa mawazo haya ndio Paulo alifanya kazi kumhudumia Mungu. Je, mawazo na madhumuni kama hayo hayatoki kwa asili ya Shetani? Watu wana asili ya shetani, kwa hiyo ulimwenguni watafuatilia maarifa, hadhi, kujifunza, na mafanikio ya dunia; nyumbani mwa Mungu, watatafuta kujitumia kwa ajili ya Mungu, kuwa waaminifu, na hatimaye watapokea taji na baraka nyingi. Kama watu hawana ukweli baada ya kumwamini Mungu na hawajakuwa na mabadiliko katika tabia yao, basi bila shaka watakuwa kwenye njia hii—huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 602 Njia ya Imani ya Mafanikio Katika Mungu

Inayofuata: 604 Kile Ambacho Anayemwamini Mungu Anapaswa Kufuatilia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp