757 Onyo la Ushuhuda wa Ayubu kwa Vizazi vya Baadaye

1 Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka.

2 Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watakapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 756 Mshinde Shetani kwa Ukweli ili Upatwe na Mungu

Inayofuata: 758 Wamebarikiwa Wale Wanaompenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp