841 Njia ya Kukamilishwa na Mungu

1 Kadiri ufahamu wako wa maneno ya Mungu ulivyo mkuu na kadiri unavyoyatia kwenye matendo, ndivyo unavyoweza kuingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu haraka. Kupitia katika maombi, unaweza pia kufanywa mtimilifu katika maombi; pia unaweza kufanywa mtimilifu kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno hayo, na kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, unaweza kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu kila siku, unapaswa kujua kile unachokosa ndani yako, na, zaidi ya hayo, unapaswa kujua dosari yako kubwa na upungufu wako, na umwombe na kumsihi Mungu. Kwa kufanya hivyo, utafanywa mtimilifu polepole.

2 Njia za kufanywa mtimilifu: kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kuingia katika uzoefu wa maneno ya Mungu, kuja kujua kinachokosa ndani yako, kuitii kazi ya Mungu, kuzingatia mzigo wa Mungu na kuunyima mwili kwa kupitia upendo wako kwa Mungu, na kuwa na ushirika wa mara kwa mara na ndugu, ambayo yanaboresha uzoefu wako. Iwe ni maisha ya jumuiya au maisha yako binafsi, na iwe ni makusanyiko makubwa au madogo, yote yanaweza kukuwezesha kupata uzoefu na kupata mafunzo ili moyo wako uwe na utulivu mbele ya Mungu na kurudi kwa Mungu. Haya yote ni mchakato wa kufanywa mtimilifu.

3 Kuyapitia maneno ya Mungu ambayo yamesemwa kunamaanisha kuwa na uwezo wa kwa kweli kuyaonja maneno ya Mungu na kuyaruhusu yaweze kuishi kwa kudhihirishwa ndani yako ili uwe na imani kubwa na upendo kwa Mungu. Kupitia njia hii, utaondoa tabia potovu ya kishetani polepole, utaachana na motisha isiyofaa polepole, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Kadiri upendo kwa Mungu ndani yako unavyozidi kuwa mkuu—yaani, kadiri unavyozidi kufanywa mtimilifu na Mungu mara nyingi—ndivyo unayopotoshwa na Shetani kwa kiasi kidogo. Kupitia uzoefu wako wa vitendo, utaingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu polepole. Hivyo, ikiwa unataka kufanywa mtimilifu, kuzingatia mapenzi ya Mungu na kuyapitia maneno ya Mungu hasa ni muhimu sana.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 840 Lazima Uwe na Azimio na Ujasiri ili Kukamilishwa

Inayofuata: 842 Unapaswa Kutafuta Kukamilishwa na Mungu Katika Vitu Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp