845 Mungu Apata Nini Kutoka kwa Mwanadamu?

1 Katika kuwaokoa binadamu, Mungu hufanya hivyo kutokana na upendo na huruma Yake na kwa ajili ya usimamizi Wake; katika kupokea wokovu wa Mungu, jamii ya binadamu hufanya hivyo kwa sababu imeanguka hadi kiwango ambapo Mungu huzungumza binafsi tu. Mwanadamu anapoupokea wokovu wa Mungu, hii ndiyo neema kuu zaidi, na pia ni fadhila ya pekee, yaani, isingekuwa Mungu kulipa sauti tamko Lake mwenyewe, majaliwa ya jamii ya binadamu yangekuwa ni kufa. Wakati huo huo ambapo Anaikirihi jamii ya binadamu, bado Mungu yuko tayari na mwenye radhi kulipa gharama yoyote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Wakati ule ule, mwanadamu anapozungumza kwa kurudiarudia kuhusu upendo wake kwa Mungu na jinsi anavyoweka yote wakfu kwa Mungu, anaasi dhidi ya Mungu na kupokonya kila aina ya neema kutoka kwa Mungu, na hata, wakati huo huo, akimwumiza Mungu na kuuumiza moyo Wake kwa uchungu mbaya sana. Hivyo ndivyo ilivyo tofauti dhahiri kati ya asiye na ubinafsi na aliye na ubinafsi katika uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu!

2 Binadamu wanaona ikiwa rahisi kumchukulia Mungu kama mmoja miongoni mwa jamii ya wanadamu walioumbwa; uchungu na fedheha kuu kabisa ambayo binadamu wanamwumiza Mungu nayo ni hiyo hasa, Anapoonekana na kufanya kazi waziwazi, bado Mungu anakataliwa na mwanadamu na hata kusahaulika naye. Mungu huvumilia fedheha kuu zaidi ili Aweze kuiokoa jamii ya binadamu; katika kutoa kila kitu, lengo Lake ni kuwaokoa binadamu, ili Aweze kutambuliwa na binadamu. Gharama ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya haya yote ni kitu ambacho kila mtu aliye na dhamiri anapaswa kuweza kuthamini sana. Jamii ya binadamu imepata kuzungumza na kufanya kazi kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Hata hivyo, hakuna mtu ambaye amefikiria kuuliza jambo hili: Na ni nini ambacho Mungu amepata kutoka kwa binadamu? Kutoka katika kila tamko la Mungu, binadamu wameupata ukweli, wamefanikiwa kubadilika, wamepata mwelekeo katika maisha; lakini kile ambacho Mungu amekipata si zaidi ya maneno binadamu anayotumia kuonyesha kumdai kwake Mungu na minong’ono dhaifu ya sifa. Hakika hii si fidia ambayo Mungu anadai kutoka kwa mwanadamu?

Umetoholewa kutoka katika Utangulizi ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 844 Asili ya Mungu Haina Ubinafsi

Inayofuata: 846 Mungu Humkimu Kila Mtu kwa Unyamavu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki