979 Kile Afikiriacho Mungu Kuhusu Matendo ya Mwanadamu

1 Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu.

2 Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Umetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 978 Onyo la Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: 980 Umepungukia Kaisi Kipi Matakwa ya Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp