355 Mmempa Mungu Nini Kama Malipo?

1 Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu?

2 Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi?

3 Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu.

Umetoholewa kutoka katika “Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 354 Hakuna Ayejali Kumwelewa Mungu kwa Utendaji

Inayofuata: 356 Nani Awezaye Kuuelewa Moyo wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp