447 Hali ya Kawaida ni Nini?

1 Katika hali yao ya kawaida, watu hawarudi nyuma au kulemewa; wanaweza kumtafakari Mungu mioyoni mwao, kumtegemea Mungu, na kutamani sana maneno ya Mungu. Wana uwezo wa kuomba mara nyingi; wanaweza kusalia karibu na Mungu; wanaweza kuwa na mzigo kwa ajili ya maisha yao wenyewe. Wanaweza kuishi maisha ya kawaida na ya utaratibu, na mioyo yao inaweza kumgusa Mungu. Wakati mwingine kunaweza kutokea hali ambazo zinasumbua mioyo yao, lakini kupitia sala, kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, au kupitia ushirika na ndugu, wanaweza kubadili hali zao haraka. Hata ingawa wana nyakati za udhaifu, nyakati ambapo wanatekwa na mwili, wanaweza kuishi huru kutokana na haya; hawajishughulishi na hayo.

2 Jambo linapowafika, huenda pia wakapitia udhaifu wa mwili, lakini hautawatawala. Bado wataweza kutuliza mioyo yao na kusali mbele za Mungu, watatafuta mapenzi ya Mungu, wataimba nyimbo, kucheza, na kuishi maisha ya kanisa; hawatachoshwa na desturi hizi; wataendelea. Kutakuwa na nyakati ambazo watakuwa hasi, nyakati ambazo mwili ni dhaifu, lakini mara wanapotambua hilo, wanaweza kuwekwa huru kutokana na hilo. Bado wanaweza kumwomba Mungu na kubaki karibu na Yeye katikati ya uhasi. Yote haya ndiyo hufanyiza hali ya kawaida.

Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu

Iliyotangulia: 446 Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu ili Ukamilishwe

Inayofuata: 448 Hali ya Kawaida Huleta Ukuaji wa Haraka Maishani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp