Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

691 Imani ya Kweli ni Nini?

1 Je, imani inarejelea nini? Imani ni kusadiki kwa kweli na moyo wa dhati ambao wanadamu wanapaswa kumiliki wakati wao hawawezi kuona au kugusa kitu, wakati kazi ya Mungu haiambatani na dhana za binadamu, wakati inazidi uwezo wa binadamu. Hii ndiyo imani Ninayozungumzia. Watu wanahitaji imani katika nyakati za shida na usafishaji, na pamoja na imani huja usafishaji. Hivi havichanguliki. Haijalishi jinsi Mungu anavyofanya kazi au ni aina gani ya mazingira uliyomo, ikiwa unaweza kufuatilia maisha, kuendeleza kazi ya Mungu ndani yako, na kuufuatilia ukweli na ikiwa una uelewa wa matendo ya Mungu na unaweza kutenda kulingana na ukweli, basi hii ni imani yako ya kweli na hii inaonyesha kuwa hujapoteza tumaini kwa Mungu.

2 Kama tu bado unaweza kuufuatilia ukweli kupitia usafishaji, unaweza kumpenda Mungu kwa kweli na usiwe na mashaka na Yeye, kama haijalishi Anachokifanya bado unatenda ukweli kumridhisha Yeye na unaweza kutafuta mapenzi Yake kwa kina na kujali mapenzi Yake, basi hii inamaanisha una imani ya kweli katika Mungu. Awali, wakati Mungu alisema kwamba ungetawala kama mfalme, ulimpenda, na wakati Alijionyesha hadharani kwako, ulimfuata. Lakini sasa Mungu amejificha, huwezi kumwona, na shida zimekujia. Kwa wakati huu, je, unapoteza matumaini katika Mungu? Hivyo wakati wote ni lazima ufuatilie maisha na kutafuta kuridhisha mapenzi ya Mungu. Hii inaitwa imani ya kweli, na ni aina ya upendo ulio wa kweli na mzuri zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Uko Tayari Kumpa Mungu Upendo Ulio Moyoni Mwako

Inayofuata:Unapaswa Kumwiga Petro

Maudhui Yanayohusiana