600 Mtu wa Aigan Gani Hawezi Kuokolewa?

1 Kama mnaweza kuokolewa hakutegemei jinsi ulivyo na sifa za kustahili, au ni umefanya kazi kwa miaka ngapi, sembuse idadi ya sifa ambazo unazo. Kunategemea na ikiwa kumekuwa na matokeo yoyote katika kufuatilia kwako. Hata kama umetumia miaka mingi kuzurura mitaani, ina maana gani? Ushahidi wako uko wapi? Uchaji wako kwa Mungu ni mdogo sana kuliko upendo wako wa wewe na hamu zako za tamaa—mtu kama huyu si mpotovu? Ungewezaje kuwa mfano na kielelezo cha wokovu? Asili yako haibadiliki, wewe ni muasi sana, huwezi kuokolewa! Watu kama hao hawataondolewa? Je, wakati ambapo kazi Yangu inamalizika si wakati ambapo siku yako ya mwisho itakuja?

2 Nimefanya kazi nyingi sana na kusema maneno mengi kati yenu—ni kiasi gani cha hayo kilichoingia ndani ya masikio yenu? Ni kiasi gani cha hayo ambacho mmewahi kutii? Wakati kazi Yangu itaisha ndio pia utakuwa wakati unapoacha kunipinga na kusimama dhidi Yangu. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu—uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa?

3 Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 599 Mungu Daima Anamsubiri Mwanadamu Kumrudia

Inayofuata: 601 Mwisho Wako Utakuwa Upi?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki