612 Kinachohitajika ili Kuwa Mtu Anayemtumikia Mungu

1 Mtu anayemhudumia Mungu kwa ukweli ni Yule anayeitafuta roho ya Mungu na anayefaa kutumiwa na Mungu na anayeweza kuacha dhana zake za kidini. Ikiwa unataka kunywa na kula kwako kwa maneno ya Mungu kuzaa matunda, basi ni sharti uache dhana zako za kidini. Ikiwa unataka kumhudumia Mungu, basi ni muhimu zaidi kuacha dhana zako za kidini na kutii maneno ya Mungu kwa kila unachokifanya. Hizi ni sifa za lazima kwa yeyote anayemhudumia Mungu. Ukikosa ufahamu huu, punde tu unapohudumu utasababisha hitilafu na usumbufu, na ukiendelea kushikilia dhana zako, basi bila shaka utagongwa chini na Mungu, usinyanyuke daima. Chukulia wakati wa sasa kama mfano. Mengi ya matamshi na kazi za leo hazilingani na Biblia pamoja na kazi zilizofanywa na Mungu hapo awali, na kama huna nia ya kutii, basi unaweza kuanguka wakati wowote.

2 Ikiwa unataka kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kuziacha kwanza dhana zako za kidini na urekebishe mitazamo yako. Mengi ya yale yatakayosemwa katika siku za usoni hayatalingana na yaliyosemwa zamani na ikiwa sasa unakosa nia ya kutii, hutaweza kuipita njia iliyo mbele yako. Ikiwa njia moja ya Mungu ya kufanya kazi imechipuka ndani yako na huachii dhana zako, basi njia hii itakuwa dhana zako za kidini. Ikiwa kile Mungu Alicho kimekita mizizi ndani yako, basi umepata ukweli, na ikiwa maneno na ukweli wa Mungu unaweza kuwa maisha yako, kamwe hutakuwa na dhana kuhusu Mungu. Walio na ufahamu wa kweli kuhusu Mungu hawatakuwa na dhana na hawatatii mafundisho ya kidini.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 611 Kumhudumia Mungu Unapaswa Kumpa Moyo Wako

Inayofuata: 613 Kinachohitajika ili Kuliongoza Kanisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp