476 Kile Vijana Hawana Budi Kufuatilia

Hawapaswi kuwa bila ukweli, hasa vijana hawapaswi kuwa bila azimio la utambuzi katika masuala, na la kutafuta haki na ukweli.

1 Macho ambayo yamejaa uongo na chuki bila sababu kwa watu siyo wanayopaswa kuwa nayo vijana, na wale wanaotekeleza vitendo vya uharibifu, vinavyochukiza mno hawapaswi kuwa vijana. Hawapaswi kuwa bila maadili, matarajio, au tabia ya maendeleo ya shauku; hawapaswi kuvunjika moyo juu ya matarajio yao wala hawapaswi kupoteza matumaini maishani au kupoteza imani katika siku zijazo; wanapaswa kuwa na uvumilivu kuendelea na njia ya ukweli ambayo sasa wamechagua kufanikisha matamanio yao ya kutumia maisha yao yote kwa ajili Yangu.

2 Hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu, bali wanapaswa kusimama imara katika msimamo unaofaa. Hawapaswi tu kuzurura, bali wanapaswa kuwa na roho ya kuthubutu kujitolea mhanga na kujitahidi kwa ajili ya haki na ukweli. Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao. Vijana hawapaswi kukubali shida bila kulalamika, bali wanapaswa wawe wazi na wa kusema bila kuficha, na roho ya msamaha kwa ndugu wao.

3 Hasa vijana hawapaswi kuwa bila azimio la utambuzi katika masuala, na la kutafuta haki na ukweli. Yale mnayopaswa kufuata ni mambo yote mazuri na mema, na mnapaswa kupata uhalisi wa mambo yote mazuri, na pia kuwajibika juu yaa maisha yenu—hampaswi kuyachukulia kwa wepesi.

Umetoholewa kutoka katika “Maneno kwa Vijana na kwa Wazee” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 475 Maisha ya Maana Zaidi

Inayofuata: 477 Yachukulie Maneno ya Mungu kama Msingi wa Matendo Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp