38 Mungu Mwenyewe Akujapo Duniani

1 Wakati watu Wangu, kupitia kwa kazi Yangu, wanatukuzwa pamoja na Mimi, wakati huo maficho ya joka kubwa jekundu yatafichuliwa, matope yote na uchafu kufagiliwa mbali, na maji machafu, yaliyokusanyika kwa miaka mingi, kukaushwa na moto Wangu unaochoma, yasikuwepo tena. Hapo joka kubwa jekundu litaangamia katika ziwa la moto wa jehanamu. Je, kweli unayo nia ya kusalia chini ya ulinzi Wangu ili usinyakuliwe na joka? Je, kweli unachukia mbinu yake ya udanganyifu? Nani ambaye anaweza kuwa shahidi Wangu wa dhati? Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, na kwa sababu ya mpango Wangu mzima wa usimamizi, ni nani anayeweza kutoa nguvu zake zote?

2 Leo, wakati ambao ufalme upo katika ulimwengu wa wanadamu, ni wakati ambao Nimekuja binafsi miongoni mwa binadamu. Kama haingekuwa hivyo, je, kuna yeyote ambaye anaweza kujitokeza aende kwenye uwanja wa vita kwa niaba Yangu bila hofu yoyote? Ndipo ufalme uweze kuchukua mkondo, ili moyo Wangu uweze kuridhika, na tena, ili siku Yangu iweze kuja, ili wakati uweze kuja ambapo mambo mengiya uumbaji yamezaliwa upya na kukua kwa wingi, ili kwamba mwanadamu aweze kuokolewa kutoka kwenye bahari ya mateso, ili siku inayofuata iweze kuja, na ili iwe ni ya ajabu, yenye kutoa maua na kushamiri, na tena, ili starehe ya siku za usoni itimizwe, binadamu wote wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuwacha chochote katika kujitoa sadaka wenyewe kwa ajili Yangu. Je, hii si ishara kwamba ushindi tayari ni Wangu, na alama ya kukamilika kwa mpango Wangu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 15” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 37 Kusonga kwa Kazi ya Mungu Ulimwenguni

Inayofuata: 39 Mungu Amemleta Mwanadamu Katika Enzi Mpya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp