1002 Mungu Arudipo Sayuni

1 Wakati kila kitu kiko sawa, hiyo ndiyo siku ambayo Nitarudi Sayuni, na siku hii itakumbukwa na watu wote. Nitakaporudi Sayuni, vitu vyote duniani vitakuwa kimya na vitu vyote duniani vitakuwa na amani. Wakati ambapo Nimerudi Sayuni, kila kitu kitarejelea sura yake ya awali. Wakati huo, Nitaianza kazi Yangu katika Sayuni, Nitawaadhibu waovu na kuwatuza wazuri, Nitaleta mamlakani haki Yangu nami Nitatekeleza hukumu yangu. Nitatumia maneno Yangu kukamilisha kila kitu na kumfanya kila mtu na kila kitu kipitie mkono Wangu unaoadibu. Nitawafanya watu wote wauone utukufu Wangu mzima, waione hekima Yangu nzima, wauone ukarimu Wangu mzima. Hakuna mtu yeyote atathubutu kusimama kutoa hukumu kwani yote imekamilika nami. Katika hili, kila mtu ataiona heshima Yangu yote na wote watapata uzoefu wa ushindi Wangu wote kwa kuwa kila kitu kimewekwa wazi nami.

2 Kutokana na haya, mtu anaweza kuuona uwezo Wangu mkubwa vizuri, na kuyaona mamlaka Yangu. Hakuna mtu atathubutu kunikosea Mimi, hakuna mtu atathubutu kunizuia Mimi. Yote yamewekwa waziwazi nami, nani angethubutu kuficha kitu chochote? Nina uhakika wa kutomwonyesha huruma! Mafidhuli mno kama wao lazima waipokee adhabu Yangu kali na watu wabaya kabisa kama wao lazima waondolewe kutoka machoni Pangu. Nitawatawala kwa fimbo ya chuma nami Nitayatumia mamlaka Yangu kuwahukumu, bila huruma yoyote na bila kutowaudhi kabisa, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe Nisiye na hisia na ambaye ni mwadhimu na Siwezi kukosewa. Kwa asili Mimi si Mwanakondoo bali ni simba. Hakuna mtu anayethubutu kunikosea na yeyote anayenikosea Nitamwadhibu mara moja kwa kifo, bila hisia hata kidogo! Hiyo ni tabia Yangu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 120” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1001 Matamshi ya Mungu ni Ushawishi Bora kwa Mwanadamu

Inayofuata: 1003 Baada ya Mungu Kurudi Sayuni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp