997 Mungu Anapompiga Mchungaji

1 Katika siku zijazo, kila mtu ataitembea njia anayopaswa kuitembea, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ni nani atakayeweza kuwatunza wengine huku akipitia dhiki? Kila mtu ana mateso yake mwenyewe, na kila mmoja ana kimo chake mwenyewe. Hakuna kimo cha mtu yeyote kilicho sawa na cha mtu mwingine yeyote. Waume hawataweza kuwatunza wake zao, au wazazi kuwatunza watoto wao; hakuna mtu atakayeweza kumtunza mtu mwingine yeyote. Haitakuwa kama sasa, wakati ambapo kutunzana na kuhimiliana bado kunawezekana. Huo utakuwa wakati ambapo mtu wa kila aina amefunuliwa.

2 Mungu anapowapiga wachungaji, basi kondoo wa kundi watatawanyika, na wakati huo ninyi hamtakuwa na kiongozi yeyote wa kweli. Watu watakuwa wamegawanyika—haitakuwa kama sasa, wakati ambapo mnaweza kukusanyika pamoja kama mkutano. Katika siku zijazo, wale ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wataonyesha sura zao za kweli. Waume watawasaliti wake zao, wake watawasaliti waume zao, watoto watawasaliti wazazi wao, na wazazi watawatesa watoto wao—moyo wa binadamu ni usioeleweka kabisa! Kile kinachoweza kufanywa ni kwa mtu kushikilia tu kile mtu alicho nacho, na kuitembea vizuri sehemu ya mwisho ya njia. Sasa hivi, ninyi hamwoni hili wazi wazi; nyinyi nyote ni wasiofikiria mambo yajayo. Si jambo rahisi kupitia hatua hii ya kazi kwa mafanikio.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Sehemu ya Mwisho ya Njia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 996 Jinsi ya Kufuata Vizuri Hatua ya Mwisho ya Njia

Inayofuata: 998 Ujumbe wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp