989 Unauelewa Mtazamo wa Mungu Anapomwadhibu Mwanadamu

1 Kazi yangu imekuwa ya msaada sana kwa ajili yenu; kile Natarajia kupata kutoka kwenu ni moyo ulio mwaminifu na unaotia msukumo kwenda juu, lakini hadi sasa mikono Yangu bado ni tupu. Fikiria kulihusu: Wakati siku moja bado Nitakuwa na kukwazika kusikoelezeka, mtazamo Wangu kuwaelekea utakuwa upi? Je, Mimi bado Nitakuwa mwema? Je, Moyo wangu utakuwa bado mtulivu? Je, mnaelewa hisia za mtu ambaye kwa kujitahidi amelima lakini hakuvuna hata nafaka moja? Je, mnaelewa ukubwa wa jeraha la mtu ambaye amepigwa kipigo kikubwa? Je, mnaweza kuonja uchungu wa mtu aliyejawa na matumaini ambaye anafaa kuachana na mtu kwa uhusiano mbaya? Je, mmeona hasira ya mtu ambaye amekasirishwa? Je, mnaweza kujua hisia ya kulipiza kisasi kwa haraka ya mtu ambaye amekuwa akichukuliwa kwa uadui na udanganyifu?

2 Kama mnaelewa fikira za watu hawa, Nadhani haipaswi kuwa vigumu kwenu kuwaza mtazamo Mungu Atakuwa nao wakati ule wa adhabu Yake. Hatimaye, Natarajia nyote mnaweka jitihada kali kwa ajili ya hatima yenu wenyewe; hata hivyo, ni bora msitumie njia za udanganyifu katika juhudi zenu, au bado Nitasikitishwa nanyi katika moyo Wangu. Je, kusikitishwa kwa aina hii huelekea wapi? Je, hamjidanganyi wenyewe? Wale ambao hufikiria kuhusu hatima yao na bado wanaiharibu ni watu wenye uwezekano mdogo zaidi wa kuokolewa. Hata kama watu hawa watakerwa, ni nani atawahurumia? Kwa jumla, bado Niko tayari Kuwatakia muwe na hatima inayofaa na nzuri. Hata zaidi, Natarajia kwamba hakuna kati yenu atakayeanguka katika maafa.

Umetoholewa kutoka katika “Juu ya Hatima” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 988 Kumwamini Mungu Lakini Kutopata Uzima Kunaleta Adhabu

Inayofuata: 990 Wale Watu Wasiotubu Walionaswa Katika Dhambi Hawawezi Kuokolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp