458 Roho Mtakatifu Afanyapo Kazi kwa Mwanadamu

1 Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

2 Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwapa watu nuru na kuwaongoza katika maisha halisi; wakipitia maneno ya Mungu katika maisha yao tu ndipo wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu.

3 Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wao daima hufuatilia ukweli na wanamiliki ubinadamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 457 Kazi ya Roho Mtakatifu Humfanya Mwanadamu Aendelee kwa Vitendo

Inayofuata: 459 Tilia Maanani Kazi ya Roho Mtakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp