334 Siku ya Mungu Ifikapo

1 Watu wengi hata huzungumza juu ya masharti katika huduma yao kwa Mungu: Hawajali kama yeye ni Mungu au mwanadamu, na wao huzungumza juu ya masharti yao tu, na kutafuta kuridhisha tamaa zao wenyewe tu. Mnaponipikia, mnadai malipo ya huduma, wakati mnakimbia kwa ajili Yangu, mnadai pesa za mkimbiaji, mkinifanyia kazi mnadai ada ya kazi, wakati mnatoa kwa ajili ya kanisa mnadai malipo ya kurudisha nguvu, mkizungumza, mnadai malipo ya msemaji. Wale Nimehusiana nao hata hudai malipo kutoka Kwangu. Huu ndio ubinadamu wenu mkuu na wenye majivuno, na haya ndiyo matendo yanayoamrishwa na dhamiri yenu yenye joto. Hisia zenu ziko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi?

2 Siku Nitakayowapa mgongo ndiyo siku mtakayokufa, ndiyo siku ambayo giza litakuja juu yenu, na ni siku mtakayoachwa na mwanga. Siku Yangu itakapofika, Nitanyesha mvua ya moto Wangu mkali milele juu ya wana waasi walioiamsha hasira na ghadhabu yangu kali hapo awali, Nitalazimisha adhabu yangu milele juu ya wanyama wale ambao wakati mmoja waliupa lugha chafu Kwangu na wakaniacha, Nitawachoma wakati wote kwa moto wa hasira Yangu wana wa uasi waliokula na kuishi pamoja Nami lakini hawakuniamini, na wakanitukana na kunisaliti.

3 Nitawatia wote walionikasirisha kwa adhabu Yangu, Nitanyesha ghadhabu Yangu kwa ukamilifu juu ya wanyama hao waliotamani wakati mmoja kusimama kando Yangu kama visawe Vyangu ilhali hawakuniabudu wala kunitii, fimbo Ninayotumia kumgonga mwanadamu itaanguka juu ya wanyama hao waliofurahia utunzaji Wangu na siri Nilizonena, na waliojaribu kuchukua starehe ya mali ya dunia kutoka Kwangu. Sitamsamehe mtu yeyote anayejaribu kuchukua nafasi Yangu; Sitamsamehe yeyote anayejaribu kupokonya chakula na nguo kutoka Kwangu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 333 Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwaminifu kwa Maneno Yake

Inayofuata: 335 Hakuna Awezaye Kuelewa Asili ya Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp