954 Maafa Yafikapo

1 Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima.

2 Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!

Umetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 953 Tukio la Ghadhabu ya Mungu

Inayofuata: 955 Malengo na Kanuni za Matendo ya Mungu ni Wazi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp