Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno hili “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa. Baadhi ya watu wanaweza kusema, “Tumemwamini Mungu kwa miaka mingi. Tutakosaje kujua kufahamu Mungu ni nini? Je, si hili linatudunisha?” Lakini ukweli ni kwamba, ingawa kila mtu ananifuata wakati huu, hakuna yeyote anao ufahamu kuhusu kazi hii yote ya sasa. Hawatilii maanani hata maswali ya kawaida na rahisi zaidi, sembuse yale magumu sana kama yanayomhusu Mungu. Mnapaswa kujua kwamba hayo maswali ambayo mnayachukulia kuwa ya kawaida na hamjayatambua ndiyo mnayopaswa kuyajua zaidi, kwa maana mnajua tu kuufuata umati, hamyatilii maanani wala kuyajali yale ambayo mnafaa kujihami nayo. Je, mnajua kwa uhakika ni kwa nini mnapaswa kuwa na imani kwa Mungu? Je, mnajua kwa uhakika Mungu ni nini? Je, mnajua kwa uhakika binadamu ni nini? Kama mwanadamu ambaye yuko na imani kwa Mungu, iwapo huelewi mambo haya, je, hupotezi hadhi ya mwumini wa Mungu? Kazi Yangu leo ni hii: kuwafanya watu waelewe umuhimu wao, kuelewa yote Ninayoyafanya, na kufahamu uso wa kweli wa Mungu. Hiki ndicho kitendo cha kufunga cha mpango Wangu wa usimamizi, hatua ya mwisho ya kazi Yangu. Ndiyo maana Nawaambia yote kuhusu mafumbo ya maisha mapema, ili nyote muweze kuyakubali kutoka Kwangu. Kwa kuwa hii ndiyo kazi ya nyakati za mwisho, lazima Niwaeleze ukweli wa maisha jinsi ilivyo kwa maana hamjawahi kuyakubali, hata ikiwa huwezi kuyakubali na kuyashika, kwa maana mmepungukiwa sana na hamna matayarisho ya kutosha. Ninataka kumalizia kazi Yangu, kukamilisha kazi yote Ninayopaswa kukamilisha, na kuwafahamisha kikamilifu kuhusu yale Ninayowatuma mfanye, msije mkapotoka tena na kuanguka katika mitego ya mwovu giza linapoingia. Kuna njia nyingi zaidi ya ufahamu wenu, maneno mengi msiyoelewa. Ninyi ni wapumbavu sana. Nazijua hali zenu na upungufu wenu vema. Kwa hivyo, ingawa kuna maneno mengi ambayo hamtaweza kuyaelewa, bado Ninataka kuwaambia ukweli huu wote ambao hamjawahi kuuchukua—kwa kuwa kila mara Ninahofu iwapo, katika hali yenu ya sasa, mtaweza kusimama na kutoa ushuhuda Kwangu. Sio kwamba Nawadhalilisha. Nyote mmekuwa wanyama ambao hawajapitia mafunzo Yangu ya rasmi, na hili ni jambo ambalo linaleta shauku kuhusu kiasi cha utukufu ulio ndani yenu. Ingawa Nimetumia nguvu nyingi kushughulika juu yenu, inaonekana kuwa vipengele vizuri ndani yenu havipo kabisa, ilhali dalili za uovu zinaweza kuhesabika kwa vidole na zinatumika tu kama shuhuda za kumwaibisha Shetani. Takriban kila kitu kingine ndani yenu ni sumu ya Shetani. Mnaonekana Kwangu ni kama ambao mmepita kiwango cha kuokolewa. Kama mambo yalivyo, Naziangalia baadhi ya maonyesho na mienendo yenu, na hatimaye, Najua vimo vyenu halisi. Hiyo ndiyo maana Nina wasiwasi kwa sababu yenu: Akiachwa kuishi maisha peke yake, je, mwanadamu atapata kuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyo sasa? Je, hamna wasiwasi kuhusu hali zenu za kitoto? Mnaweza hakika kuwa kama watu wateule wa Uyahudi, kuwa waaminifu Kwangu pekee Yangu katika kila hali? Kile mnachodhihirisha sio mchezo wa watoto ambao wametangatanga kutoka wazazi wao, bali ni unyama unaoonekana katika wanyama ambao wako mbali na mjeledi wa mchungaji wao. Mnapaswa kujua hali yenu halisi, ambayo pia ni udhaifu mlio nao nyote, ambao ni ugonjwa mlio nao nyote. Kwa hivyo ombi Langu la pekee kwenu ni kwamba muwe na ushahidi Kwangu. Msije katika hali yoyote kuyaruhusu maradhi ya zamani kuchipuka tena. Jambo la muhimu zaidi ni kutoa ushuhuda. Hicho ndicho kiini cha kazi Yangu. Mnafaa kuyakubali maneno Yangu jinsi Maria alivyokubali ufunuo wa Yehova uliomjia kupitia kwenye ndoto, kuamini na kisha kutii. Hili pekee ndilo linakubalika kama kuwa mtakatifu. Kwa maana ni ninyi ndio mnasikia neno Langu zaidi, na ambao wamebarikiwa zaidi na Mimi. Ninawapa mali Yangu yote ya thamani, kuwakabidhi kila Nilicho nacho. Hali yenu na ile ya Wayahudi, hata hivyo, ni tofauti kabisa, ni kama nchi mbili tofauti. Lakini mkilinganishwa nao, mnapokea baraka nyingi zaidi yao. Huku wao wakisubiri kwa hamu ili kujitokeza Kwangu, muda mwingi Nimekuwa na ninyi, kutumia utajiri Wangu kwa pamoja. Kwa ulinganisho, ni nini kinachowapa haki ya kunifokea na kuzozana na Mimi na kudai sehemu za mali Yangu? Hampati vya kutosha? Ninawapa vingi sana, lakini Mnachonipa ni huzuni wa kuvunja moyo na dhiki na chuki isiyokomeshwa na kutoridhika. Mnakuwa wazushi sana, ilhali bado mnaiamsha huruma Yangu. Kwa hivyo sina la kufanya ila kuizima chuki Yangu yote na kunena kupinga Kwangu kwenu tena na tena. Katika hii miaka elfu kadhaa ya kazi Yangu, Sikuwa Nimewahi kuleta pingamizi kwa mwanadamu awali kwa kuwa Nilikuwa Nimegundua kwamba katika historia ya kukua kwa mwanadamu, wale waongo zaidi miongoni mwenu ndio wanaofahamika zaidi. Wao ni kama urithi wa thamani ambao umeachiwa wewe na “babu” maarufu wa zama za kale. Jinsi gani Ninavyochukia wale nguruwe na mbwa ambao wana upungufu wa ubinadamu. Hamna hisia kabisa! Tabia zenu ni zenye uovu sana! Mioyo yenu ni migumu mno! Iwapo Ningepeleka haya maneno Yangu na hii kazi Yangu kwa Wayahudi, Ningekuwa nimeshapata utukufu muda mrefu uliopita. Lakini sio hivyo miongoni mwenu. Miongoni mwenu kuna tu kutojali kwa kikatili, madharau yenu, na visingizio vyenu. Hamna hisia na hamna thamani yoyote kabisa!

Mnafaa kutoa kila kitu chenu kwa ajili ya kazi Yangu. Mnapaswa kufanya kazi inayonifaidi Mimi. Nataka Niwaambie kuhusu yale yote ambayo hamna ufahamu kamili kuyahusu ili muweze kupata yale yote mnayokosa kutoka Kwangu. Hata ingawa kasoro zenu ni nyingi kiasi kwamba haziwezi kuhesabika, Nina nia ya kuendelea kufanya kazi Ninayopaswa kuwa Nikifanya kwenu, kuwapa huruma Zangu za mwisho ili mpate kufaidika kutoka Kwangu, na mpate utukufu ambao hauko ndani yenu na ambao dunia haijawahi kuuona. Nimefanya kazi kwa miaka mingi sana, ilhali hakuna yeyote miongoni mwa binadamu ambaye amewahi kunijua. Nataka kuwaambia siri ambazo sijawahi kumwambia mtu yeyote yule.

Miongoni mwa binadamu, Nilikuwa roho ambaye hawakuweza kuona, Roho ambayo hawangeweza kuigusa. Kwa sababu ya hatua Zangu tatu za kazi duniani (kuumba ulimwengu, ukombozi, na kuiharibu), Naonekana miongoni mwao katika nyakati tofauti (kamwe sio hadharani) ili kutenda kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Mara ya kwanza Nilipokuja miongoni mwa binadamu ilikuwa katika Enzi ya Ukombozi. Bila shaka Nilikuja miongoni mwa jamii ya Wayahudi; kwa hivyo watu wa kwanza kumwona Mungu Akija ulimwenguni walikuwa Wayahudi. Sababu Yangu ya kufanya kazi hii mwenyewe ilikuwa kwa sababu Nilitaka kutumia kupata mwili Kwangu kama sadaka ya dhambi katika kazi Yangu ya ukombozi. Kwa hivyo watu wa kwanza kuniona Mimi walikuwa Wayahudi wa Enzi ya Neema. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza Mimi kufanya kazi Nikiwa katika mwili. Katika Enzi ya Ufalme, kazi Yangu ni kushinda na kutakasa, kwa hivyo kwa mara nyingine Nafanya kazi ya uchungaji katika mwili. Hii ni mara Yangu ya pili kufanya kazi katika mwili. Katika hatua mbili za mwisho za kazi, wanachokutana nacho watu si tena Roho asiyeonekana, asiyeshikika, bali ni mwanadamu ambaye ni Roho Aliyefanyika mwili. Hivyo machoni pa binadamu, Nilikuwa tena mtu asiye na sura wala hisia za Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu ambaye watu huona, si wa kiume pekee, bali pia ni wa kike, kitu ambacho ni cha kushtua na kushangaza kwao. Muda baada ya muda, kazi Yangu ya ajabu huziondoa imani za kale ambazo zimekuwa kwa miaka mingi sana. Watu hushangazwa! Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyeongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa na binadamu, na tofauti kwamba mmoja alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike. Katika hii miaka yote, ambayo watu wamekiona si Roho pekee na mwanamume, bali pia vitu vingi visivyoambatana na fikira za binadamu, na kwa hivyo hawawezi kunielewa kikamilifu kamwe. Wanashinda wakiniamini mara nyingine na mara nyingine wakiwa na shaka kunihusu, na iwapo Nipo kwa uhakika na ilhali Mimi ni ndoto ya mawazo. Ndio maana mpaka siku ya leo, watu hawatambui Mungu ni nini. Unaweza kweli kunieleza kwa sentensi moja? Unaweza kweli kusema kwa uhakika kwamba “Yesu si mwingine ila ni Mungu, na Mungu si mwingine ila Yesu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu si mwingine bali Roho na Roho si mwingine bali ni Mungu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu ni binadamu tu aliyevalia mwili?” Kwa kweli una ujasiri wa kusema kuwa “Taswira ya Yesu ni taswira kubwa ya Mungu?” Unaweza kuelezea kwa umakinifu tabia ya Mungu na umbo kwa uwezo wa kipawa chako cha maneno? Unaweza hakika kuthubutu kusema kuwa Mungu Aliumba kiume pekee, sio kike, kwa mfano Wake mwenyewe? Ukisema hivi, basi kusingekuwepo na mwanamke miongoni mwa wateule Wangu na hata zaidi wanawake wasingekuwa aina miongoni mwa wanadamu. Sasa, unajua hakika Mungu ni nini? Je, Mungu ni binadamu? Je, Mungu ni Roho? Je, Mungu kwa uhakika ni wa kiume? Je, ni Yesu pekee Anayeweza kukamilisha kazi ambayo Ninataka kufanya? Ukichagua moja tu kati ya haya kujumuisha kiini Changu, basi utakuwa muumini mjinga kabisa. Nikifanya kazi kama mwili uliopatikana mara moja tu, je, unaweza kuniwekea mipaka? Je, unaweza hakika kuniangalia mara moja na ukajua yaliyo ndani Yangu? Je, unaweza hakika kunieleza kikamilifu kwa mujibu tu wa yale ambayo umeyafahamu wakati wa maisha yako? Na iwapo katika kuingia Kwangu kwa mwili mara mbili Nafanya kazi inayofanana, utanichukulia vipi? Unaweza kuniacha milele msalabani nikiwa na misumari? Je, Mungu anaweza kuwa wa kawaida jinsi unavyosema?

Ijapokuwa imani yenu ni ya kweli kabisa, hakuna kati yenu anayeweza kueleza kunihusu kabisa, na hakuna kati yenu anayeweza kushuhudia uhalisi mnaouona. Tafakari kuhusu jambo hili. Sasa hivi wengi wenu hamyatimizi wajibu wenu, mkifuata vitu vya mwili, mkishibisha mwili na kuburudika kwa mwili. Mnamiliki ukweli mdogo. Mnawezaje basi kushuhudia yote ambayo mmeyaona? Mna uhakika kuwa mtakuwa mashahidi Wangu? Iwapo siku moja utashindwa kushuhudia yote ambayo umeyaona leo, basi utakuwa umepoteza jukumu la kiumbe aliyeumbwa. Hakutakuwa na maana kabisa ya kuwepo kwako. Utakuwa hustahili kuwa binadamu. Mtu anaweza hata kusema kuwa wewe si binadamu! Nimefanya kazi isiyo na kifani kwako. Lakini kwa sababu kwa sasa hujifunzi chochote, hujui chochote, na kufanya kazi bure, Nikitaka kuipanua kazi Yangu utatazama bila kuelewa, bila kusema chochote na kuwa asiye na umuhimu wowote. Hiyo haitakufanya mtenda dhambi mkubwa zaidi? Wakati huo utakapofika, je, hutakuwa na majuto makuu? Hutazama katika huzuni kubwa? Sifanyi kazi hii yote sasa kwa sababu ya kukosa la kufanya na uchoshi, bali kuweka msingi kwa kazi Yangu ya baadaye. Sio kwamba Niko katika njia isiyopitika na Nahitajika kubuni kitu kipya. Unafaa kuelewa kazi ambayo Nafanya; si kitu kinachofanywa na mtoto anayecheza mtaani, bali ni kwa uwakilishi wa Baba Yangu. Unafaa kujua kuwa si Mimi tu Ninayefanya haya yote pekee Yangu bali Namwakilisha Baba Yangu. Wakati uo huo, jukumu lako ni kufuata, kuheshimu, kubadilika, na kushuhudia kwa makini. Unachofaa kuelewa ni kwa nini unafaa kuniamini. Hili ndilo swali muhimu kwa kila mmoja wenu kuelewa. Baba Yangu, kwa ajili ya utukufu Wake, ndiye Aliyewachagua ninyi kwa ajili Yangu kutoka wakati Alipoumba dunia. Haikuwa kwa ajili ya kitu kingine ila kwa ajili ya kazi Yangu na kwa ajili ya utukufu Wake, ndio maana Aliweka hatima yenu awali. Ni kwa sababu ya Baba Yangu ndio unaniamini; ni kwa sababu ya Baba Yangu kukuamua kabla ndio maana unanifuata Mimi. Hakuna kati ya haya ambayo ulichagua kwa hiari yako mwenyewe. La muhimu zaidi ni kwamba muelewe kuwa ninyi ni wale ambao Baba Yangu alinitawazia kwa ajili ya kushuhudia kwa niaba Yangu. Kwa sababu Aliwatawaza Kwangu, mnafaa kuzifuata njia ambazo Natawaza kwenu na njia na maneno ambayo Ninawafunza, kwani ni jukumu lenu kuzifuata njia Zangu. Hili ndilo kusudi la asili la imani yenu Kwangu. Kwa hivyo Nawaambieni, ninyi ni watu tu ambao Baba Yangu Alitawaza Kwangu ili mfuate njia Zangu. Hata hivyo, mnaamini tu Kwangu; ninyi si wa Kwangu kwa sababu ninyi si wa familia ya Wayahudi bali ni wa joka la zama. Kile Ninachowasihi ni muwe washahidi Wangu, lakini leo lazima mtembee kwa njia Zangu. Haya yote ni kwa ajili ya ushuhuda wa baadaye. Mkihudumu tu kama watu ambao wanasikiliza njia Zangu pekee, basi hamtakuwa na thamani yoyote na umuhimu wa Baba Yangu kuwatawaza Kwangu utapotea. Ninachosisitiza kuwaambia ni hiki: Mnapaswa kutembea katika njia Zangu.

Iliyotangulia: Ufahamu wako wa Baraka ni Upi?

Inayofuata: Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp