1016 Ufalme Unapokuja Kikamilifu

Ufalme utakaposhuka duniani kabisa, watu wote watapata tena mfano wao wa asili. Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Hili linaonyesha kwamba siku ambayo Mungu atapata utukufu kamili ndiyo siku ambayo mwanadamu atafurahia pumziko lake; watu hawakimbii huku na huko tena kutokana na usumbufu wa Shetani, dunia inaacha kuendelea mbele, na watu wanaishi katika pumziko—kwa kuwa idadi kubwa mno ya nyota angani zinafanywa upya, na jua, mwezi, na nyota, na kadhalika, na milima na mito yote iliyo mbinguni na duniani, vyote vinabadilishwa. Na kwa kuwa mwanadamu amebadilika, na Mungu amebadilika, kwa hiyo, pia, vitu vyote vinabadilika. Hili ndilo lengo la msingi la mpango wa usimamizi wa Mungu, na ule ambao utatimizwa hatimaye.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 20” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1015 Baraka Kuu Zaidi Ambayo Mungu Anaweka Juu Ya Mwanadamu

Inayofuata: 1017 Ahadi ya Mwisho ya Mungu kwa Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp