18 Saluti ya Ufalme Inaposikika

1 Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu jinsi ambavyo binadamu hutenda; badala yake, Nimeshuka duniani ili Nitekeleze kazi Yangu binafsi, jambo ambalo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha. Punde ujenzi wa ufalme ulipoanza, Mimi nikiwa mwili nilianza rasmi kutekeleza huduma Yangu; yaani, Mfalme wa ufalme rasmi Alichukua ukuu wa mamlaka Yake makuu. Kutokana na hili ni dhahiri kwamba mshuko wa ufalme katika ulimwengu wa binadamu. Kotekote katika ulimwengu, binadamu wote hukaa chini ya upendo Wangu, huruma Yangu, lakini pia binadamu wote hukaa chini ya hukumu Yangu, na vivyo hivyo chini ya majaribio Yangu. Nimekuwa mwenye huruma na upendo kwa wanadamu, hata wakati watu wote walikuwa wamepotoshwa kwa kiwango fulani; Nimegawa kuadibu kwa wanadamu, hata wakati watu wote walinyenyekea mbele ya kiti Changu cha enzi. Lakini, yupo binadamu yeyote ambaye hayuko katikati ya mateso na usafishaji Niliotuma?

2 Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambao pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, inatetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe katika taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kisha kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaanzishwa duniani. Wakati huu, Naanza kutuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hili pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 10” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 17 Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu

Inayofuata: 19 Mfalme wa Ufalme ni Mshindi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp