690 Lazima Utafute Mapenzi ya Mungu Ugonjwa Unapotokea

1 Mateso ya ugonjwa yanapokupata, unapaswa kuyapitiaje? Unapaswa kuja mbele za Mungu kuomba, ukitafuta kuelewa mapenzi Yake na kuchunguza umefanya makosa ya aina gani au ni upotovu wa gani ambao bado haujasuluhisha. Huna budi kuteseka kimwili. Ni kwa kupunguzwa nguvu kupitia mateso tu ndipo watu wanaweza kukoma kuwa watovu wa nidhamu na kuishi mbele za Mungu kila wakati. Watu wanapohisi kufadhaika, wao husali kila mara, wakitafakari ikiwa wametenda jambo lolote baya au jinsi ambavyo labda wamemkosea Mungu. Jambo hili ni la manufaa kwao. Watu wanapopata maumivu na majaribio makubwa, hakika hayafanyiki kwa bahati.

2 Ikiwa watu ni wagonjwa au wenye afya njema, mapenzi ya Mungu yako kazini. Wakati ambapo wao ni wagonjwa na hawayajui mapenzi ya Mungu, hawatajua jinsi ya kutenda. Watadhani kuwa haya ni matokeo ya upumbavu wao. Hawajui vipi kuwa nia njema ya Mungu iko kazini? Unapopata ugonjwa mkubwa unaokufanya uhisi ni bora ufe, haifanyiki kwa bahati. Wakati wa wokovu wa Mungu kwa wanadamu, Roho Mtakatifu huandamana tu na maisha ya watu, Akiwapa nuru na kuwaangazia? Mungu pia Atajaribu kuwasafisha watu. Wanaweza kutakaswa ikiwa tu watateseka sana, na wakati huo tu ndipo tabia yao ya maisha inaweza kubadilishwa.

3 Mungu huwajaribu watu vipi? Yeye huwasafisha kupitia mateso. Majaribio ni mateso, na wakati wowote kunapokuwa na majaribio, yanaambatana na mateso. Kusingekuwa na majaribio, watu wangeteseka vipi? Na wasingeteseka, wangebadilikaje? Majaribio yanaambatana na mateso na hiyo ndiyo kazi ya Roho Mtakatifu. Wanadamu wamepotoka kabisa, na wasipoteseka, watasahau mahali pao ulimwenguni. Wasipoteseka, hawatakuwa na Mungu mioyoni mwao. Kufanya ushirika tu juu ya ukweli hakuwezi kutatua tabia potovu ya watu; lazima kufanyike kupitia majaribio na usafishaji.

Umetoholewa kutoka katika “Lazima Uangalie Masuala Yote kwa Makini kwa Mtazamo wa Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 689 Kupitia Upogoaji na Ushughulikiwaji ni kwa Maana Sana

Inayofuata: 691 Kuja kwa Magonjwa ni Upendo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp