353 Uko Wapi Ushahidi wa Kulingana Kwako na Mungu

1 Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu anayeepuka kuathiriwa na hila yenu, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe.

2 Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu?

3 Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 352 Nani Analingana na Mungu?

Inayofuata: 354 Hakuna Ayejali Kumwelewa Mungu kwa Utendaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp