371 Nani Awezaye Kutunza Mapenzi ya Mungu?

1 Mwanadamu ameshuhudia upendo Wangu, mwanadamu amenitumikia kwa dhati, na mwanadamu amenitii kwa kweli, akinifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Ilhali jambo hili haliwezi kutimizwa na watu ; wanalia tu katika roho zao kana kwamba wamenyakuliwa na mbweha mwenye njaa, na wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, wakinililia bila kukoma. Lakini mwishowe, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba.

2 Ninakumbuka jinsi ambavyo watu wa kale waliweka ahadi mbele Zangu, wakiapa kwa mbingu na dunia mbele Zangu kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo, kigumu kuvumilia. Kwa sababu ya azimio lao, mara nyingi niliwapa watu msaada. Mara nyingi, wanadamu wamekuja mbele Zangu kunitii, mienendo yao ya kupendeza isiyoweza kusahaulika. Mara nyingi, wamenipenda bila kutikisika katika uaminifu wao, bidii yao ikiwa ya kupendeza.

3 Mara nyingi, wamenipenda hadi kiwango cha kuhatarisha maisha yao, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe—na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara nyingi, wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kumekuwa na nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama kitu kinachothaminiwa, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hata hivyo, kile kilicho fikirani Mwangu hakiwezi kueleweka na mwanadamu.

4 Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Lakini, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani anayeweza kutibu kidonda kilicho moyoni Mwangu? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayejitolea kushirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini kwamba hakuna lolote kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, haya yote si kwa sababu ya mwanadamu kupotoshwa na adui yake?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 27” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 370 Kinachomhuzunisha Mungu Zaidi

Inayofuata: 372 Nani Amewahi Kuelewa Moyo wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp