372 Nani Amewahi Kuelewa Moyo wa Mungu?

1 Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wabinafsi sana Kwake, hajawahi kufurahia utajiri wote wa duniani, Amejitoa kikamilifu, moyo wa upendo wa dhati kwa mwanadamu, Amejirithisha mzima kwa mwanadamu—ni nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, shida zote mbaya Alizozipitia ni mwanadamu amempatia Yeye, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Amezikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata kidogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Ni nani amewahi kumwonyesha huruma yoyote?

2 Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hajawahi kuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hajawahi kuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa rafiki wa karibu? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wao? Je, Amekwishawahi kufurahia moja ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumpatia faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumwonyesha angalau maadili hata kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja Naye? Mwanadamu bado hajaacha kumwomba Yeye; anapeleka tu maombi Kwake bila hata haya, kana kwamba kuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alipaswa kuwa ng’ombe au farasi wake, na Alipaswa kumpatia mwanadamu kila kitu chake. Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutoka katika Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua?

3 Ukweli upo wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli ipo wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuwa miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Inawezekanaje mwanadamu kuvumilia uwepo wa Mungu? Anawezaje kuvumilia kuruhusu mwanga kuondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Je, kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kurekebisha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kufanya majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na mwanadamu kwa uwezo wako wote. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikiwa ni pamoja na utukufu Wake!

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 371 Nani Awezaye Kutunza Mapenzi ya Mungu?

Inayofuata: 373 Kwa Nini watu Hawampendi Mungu kwa Kweli?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp