163 Sababu ya Kristo Kuja Kufanya Kazi Duniani

1 Ingawa Kristo duniani Anaweza kufanya kazi kwa niaba ya Mungu Mwenyewe, hajakuja na nia ya kuonyesha watu wote mfano Wake katika mwili. Yeye hajakuja kwa watu wote kumwona; Anakuja kwa ajili ya kuwaruhusu binadamu kuongozwa na mkono Wake, na hivyo kuingia katika enzi mpya. Kazi ya mwili wa Kristo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu Mwenyewe, yaani, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika mwili, na si ili kuwawezesha binadamu kuelewa kikamilifu kiini cha mwili Wake. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, haiwezi kuzidi yanayoweza kupatwa na mwili. Haijalishi jinsi Anavyofanya kazi, anafanya hivyo katika mwili na ubinadamu wa kawaida, na wala hafichui kwa kikamilifu kwa mwanadamu uso wa kweli wa Mungu. Zaidi ya hayo, kazi Yake katika mwili kamwe sio isiyo ya kawaida au isiyokadirika kama mwanadamu anavyodhani.

2 Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo.

Mungu hupata mwili tu kukamilisha kazi ya mwili, na sio tu kuwaruhusu watu wote kumwona. Badala yake, Yeye huacha kazi Yake ithibitishe utambulisho Wake, na kuruhusu Anachofichua kushuhudia dutu Yake. Dutu Yake haikosi msingi; utambulisho Wake haukukamatwa na mkono Wake; huamuliwa kwa kazi Yake na dutu Yake.

Umetoholewa kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 162 Mungu Anafika Kati Yetu kwa Kimya

Inayofuata: 164 Sababu Ya Kupata Mwili Kwa Mungu katika Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp