392 Watu Wanapaswa Kumwamini Mungu kwa Moyo Unaomwogopa Mungu

1 Katika imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi sio tu kwamba hawatashindwa kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomwasi Mungu. Mungu daima yumo mioyoni mwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na daima wana moyo wa kumcha Mungu, moyo wa kumpenda Mungu. Wale wanaomwamini Mungu lazima wayafanye mambo kwa moyo wa uangalifu na wenye busara, na yote wanayoyafanya yanapasa kulingana na matakwa ya Mungu na yaweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Hawapaswi kuwa wabishi, wakifanya watakavyo, hayo hayafai katika utaratibu mtakatifu.

2 Wakati ambapo mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Watu hawawezi kuipunga bendera ya Mungu kwa madaha na kucharuka kila mahali, wakienda kwa mikogo na kutapeli kotekote; kutenda haya ni tendo la uasi la juu zaidi. Familia zina masharti zao na mataifa yana sheria zao; je, hali sio hivi hata zaidi katika nyumba ya Mungu? Je, matarajio sio makali hata zaidi? Je, hakuna amri nyingi hata zaidi za utawala? Watu wana uhuru wa kutenda watakayo, lakini amri za usimamizi za Mungu haziwezi kubadilishwa kwa hiari. Mungu ni Mungu asiyewaruhusu watu kumkosea; Yeye ni Mungu anayewaua watu. Je, watu kweli hawajui hili tayari?

Umetoholewa kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 391 Kipaumbele cha Juu cha Imani Katika Mungu

Inayofuata: 393 Fuata Njia Iongozwayo na Roho Mtakatifu Katika Imani Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp