701 Mabadiliko Katika Tabia ni Nini?

1 Inapofikia kujua asili ya wanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yao ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani. Wanadamu wamepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya mwanadamu imepotoka, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa jumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na humpinga Mungu.

2 Je, mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Yanafanyika wakati mpenzi wa ukweli anakubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu na kupitia kila aina ya mateso na usafisho huku anapopitia kazi ya Mungu. Mtu kama huyu anatakaswa kutokana na sumu za kishetani zilizo ndani, na kujinasua kabisa kutoka kwa tabia zake potovu, ili aweze kutii maneno ya Mungu na mipango na utaratibu Wake wote, asiasi dhidi Yake au kumpinga tena. Haya ndiyo mabadiliko katika tabia. Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi inayompinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa binadamu ni wenye kina zaidi na kutambua upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anatambua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini na asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Huyu ni mtu anayemjua Mungu; huyu ni mtu ambaye tabia yake imebadilishwa.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 700 Mabadiliko Katika Tabia Hasa ni Mabadiliko Katika Asili

Inayofuata: 702 Mabadiliko Katika Tabia Yanahitaji Kazi ya Roho Mtakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp